1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina wa Kanisa la Kianglikana wakutana Kigali

18 Aprili 2023

Mamia ya viongozi wa kihafidhina wa Kanisa la Anglikana kutoka nchi 52 wanakutana nchini Rwanda katikati mwa mpasuko wa Kanisa hilo juu ya kuunga mkono ndoa za jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4QG1M
Symbolbild I Kirche - evangelisch - katholisch
Picha: Hasenonkel/YAY Images/IMAGO

Mkutano huo wa mjini Kigali unafanyika wiki mbili baada ya kanisa hilo la England kubariki ndoa za watu wa jinsia moja. Wakosoaji kutoka afrika ni miongoni mwa wale wanaoendelea kuelezea wasiwasi wao.

Askofu Mkuu wa Rwanda Laurent Mbanda amelieleza shirika la habari la AFP kwamba uamuzi huo ulisababisha mtafaruku mkubwa unaoweza kuwa msumari wa mwisho katika kanisa hilo ambalo tayari limegubikwa na mgawanyiko.

Mpasuko huo umezidi kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni wakati maaskofu wa kihafidhina hususan kutoka Afrika na Asia wakishikilia msimamo wao wa kupinga ndoa za jinsia moja.