Waangalizi wasema uchaguzi wa Togo ulikuwa huru
30 Aprili 2024Jumuiya hiyo ya CEN-SAD ilisema kwenye taarifa yake kwamba uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira mazuri na bila matukio yoyote makubwa.
Hadi wakati jumuiya ya CEN-SAD ilipokuwa inatoa kauli yake, Tume ya Uchaguzi ya Togo ilikuwa humo haijatoa hata matokeo ya awali, kufuatia uchaguzi huo wa bunge uliofanyika baada ya wabunge kupitisha mageuzi ya katiba yanayopingwa na makundi ya upinzani yakisema yatamuongezea muda wa kukaa madarakani Rais Faure Gnassingbe.
Soma zaidi: Togo yapiga kura ya wabunge baada ya mageuzi ya kikatiba
Chama kikuu cha upinzani nchini Togo, National Alliance for Change, nacho hakikuwa kimetoa tamko lolote kuhusu mwenendo wa uchaguzi huo, lakini muungano wa upinzani (DMP), ulisema uliona hitilafu katika vituo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji wa kuanza kwa upigaji kura.
Tayari Gnassingbe ameshinda chaguzi nne tangu 2005, zote zikikosolewawa na upinzani.