Waandishi wazidi kukabiliwa na hali mbaya huko Somalia
27 Novemba 2007Matangazo
MOGADISHU.Meya wa mjini Mogadishu amepiga marufuku vyombo vya habari nchini Somalia kutangaza au kuchapisha mahojiano na wanamgambo wa kisomali.
Meya huyo Mohamed Dheere pia amepiga marufuku vyombo hivyo kuripoti juu ya harakati za kijeshi zinazoendelea pamoja na habari za wimbi la wakimbizi wanaoukimbia mji huo.
Hatua hiyo inazidisha mbinyo kwa waandishi wa habari nchini humo ambao wamekuwa wakikabiliwa na vitisho, mauaji pamoja na kukamatwa kutoka kwa pande zote mbili zinazogombana nchini humo.
Waandishi wa habari saba wameuawa mwaka huu nchini Somalia wengi kwa kupigwa risasi, mauaji ambayo bado hayajachunguzwa.