1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa habari mashakani Zanzibar?

25 Mei 2011

Mpigapicha wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Haji Bwegege, alikamatwa na askari wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wa Baraza la Manispaa hapo jana kwa kupiga picha kwenye eneo la Darajani.

https://p.dw.com/p/RQ1K
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed SheinPicha: DW

Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichotimia miezi sita kwa vikosi hivyo kuwakamata, kuwapiga, kuwachukulia vifaa vyao vya kazi na hata kuwaweka ndani kwa muda waandishi wa habari wakiwa katika kazi zao mjini Zanzibar.

Mwezi Machi mwaka huu, mwandishi wa kituo cha televisheni cha Channel 10, Munir Zakaria, alifikwa na masaibu kama haya. Jambo hili limeanza kuzua maswali miongoni mwa waandishi na wananchi, ikiwa kuwepo kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa, hakujasaidia kurekebisha tabia ya serikali kuelekea waandishi wa habari.

Mohammed Khelef amezungumza na Haji Bwegege kutaka kujua mkasa mzima ulivyokwenda na namna alivyotendewa akiwa mikononi mwa vikosi vya SMZ.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Haji Bwegege
Mhariri. Othman Miraji