1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi Kenya wapewa ushauri nasaha

Wakio Mbogho3 Agosti 2023

Mpango wa kutoa ushauri nasaha kwa waandishi wa habari nchini Kenya umeanza kutekelezwa ili kuwawezesha kukabiliana na mazingara magumu wanayoyapitia katika kazi yao, ikiwa ni pamoja na athari za afya ya akili.

https://p.dw.com/p/4UjJA
Kenia Kalobeyei  | Taphine Otieno - Content Development Coordinator
Picha: FilmAid Kenya

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeanzisha vikao vya ushauri nasaha kwa zaidi ya waandishi wa habari 30 ambao walifika na kuripoti taarifa za ajali mbaya ya Londiani iliyosababisha vifo vya watu 52.

Ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu katika eneo la kibiashara la Londiani, katika ya kaunti ya Nakuru na Kericho, na ilihusisha magari sita ya uchukuzi.

Waandishi wa habari walikuwa kati ya watu wa kwanza waliofika eneo la mkasa ili kutoa taarifa kwa umma.

Fellows Constructive Journalism Lab DW Akademie | Halima Gongo
Mwandishi wa DW mjini Mombasa Halima Gongo alishiriki kuripoti matukio ya Shakahola ambayo yamewaathiri waandishi wengi kisaikolojia na hivyo kuhitaji msaada wa ushauri nasaha.Picha: Brian Mwangi

Afisa msimamizi wa shirika la msalaba mwekundu eneo la kusini mwa bonde la ufa, Jethro Koech amesema wamegundua kuna pengo linalofaa kushughulikiwa baina ya waandishi wa habari.

Soma pia: Waandishi habari walengwa katika maandamano ya upinzani Kenya

"Tulichogndua ni kwamba waandishi wa habari wanapitia matukio mengi ya kiwewe. Hapa tunawafunza taratibu za kukabiliana na hali hiyo," alisema Koech.

""Wanapokabiliana na ile miili ya watu waliokufa, watu wanaokata roho, wanakabiliana vipi? Ni kuhakikisha kwamba kwa kuimarisha afya yao ya akili, tutawasaidia kuboresha taaluma yao.”

Athari za afya ya akili kwa waandishi wa habari wanapokosa kushughulikiwa ni kama vile mabadiliko ya tabia, matumizi ya vileo, dawa za kulevya, anasa na kuvurugika kwa familia zao.

Kulingana na mwanasaikolojia Pius Makokha waandishi wa habari hugeukia tabia hizi ili kukabiliana na magumu ya kazi yao.

Kenia I Verkehrsunfall in Londiani
Waandishi wanaoripoti matukio ya kuogofya kama ajali hii mbaya iliyotokea kwenye barabara kuu kati ya miji ya Kericho na Nakuru hubaki na kiwewe kinachoweza kuwaathiri kisaikolojia.Picha: AFPTV/AFP/Getty Images

Mara nyingi wameonyesha ukakamavu wa kuripoti majanga, matukio ya ajali, na mikasa mingine kwa muda mrefu bila kushughulikiwa afya yao ya akili, jambo analosema ni hatari kwa maisha yao na yale ya familia zao.

Soma pia: Mwandishi wa habari maarufu wa Pakistani auawa nchini Kenya

Suleiman Mbatiah mmoja wa waandishi wa habari aliyefanya kazi na vyombo vya habari nchini kama vile Nation media, The Standard na kitengo cha mawasiliano kwenye kaunti ya Nakuru, anapata huduma hii kwa mara ya kwanza licha ya kuwa kwenye sekta hii kwa miaka mingi.

Baraza la Waandishi wa habari nchini Kenya, MCK kwa ushirikiano na wahisani wengine, wameanza kutekeleza mipango ya kutoa huduma za ushauri nasaha kwa waandishi wa habari, ikiwemo pia kujumuisha masomo ya kisaikolojia kwenye mtaala wa mafunzo ya uandishi wa habari nchini Kenya.