1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wamiminika katika barabara za mjini Khartoum

7 Aprili 2023

Mamia ya waandamanaji wamefanya maandamano katika barabara za mji mkuu wa Sudan, Khartoum hapo jana baada ya mazungumzo na viongozi wa jeshi nchini humo kuhusu utawala wa kiraia kugonga mwamba.

https://p.dw.com/p/4PoSF
Sudan | Proteste in gegen die Militärherrschaft Khartoum
Picha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

Mmoja wa waandamanajii hao Waleed Adam, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba vikosi vya usalama vilikabiliana nao kwa kutumia gesi za kutoa machozi na vilipuzi vya sauti kubwa kuwatishia. Waandamanaji hao wamekataa makubaliano yoyote yanayowahusisha viongozi wa jeshi wa nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya 2021. Maandamano hayo yameongozwa na mtandao unaounga mkono demokrasia, kamati za upinzani na kuanzia Khartoum kueleka katika eneo la kiserikali. Kuanza tena kwa maandamano ya barabarani kunakuja siku moja baada ya mkutano wa makubaliano ya mwisho kati ya jeshi na vikosi vinavyounga mkono demokrasia kuahirishwa kwa mara ya pili. Hakuna tarehe mpya ya makubaliano iliyotolewa.