1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Waandamanaji wagoma kuondoa vizuizi barabarani New Caledonia

Sylvia Mwehozi
21 Mei 2024

Makundi ya watu wanaotaka kujitenga katika kisiwa cha New Caledonia yamekataa kuondoa vizuizi vya barabarani ambavyo vimekidhoofisha kisiwa hicho cha kanda ya Pasifiki ambacho ni himaya ya Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4g5A2
 New Caledonia
Magari yaliyochomwa wakati wa ghasia New CaledoniaPicha: Delphine Mayeur/AFP/Getty Images

Makundi ya watu wanaotaka kujitenga katika kisiwa cha New Caledonia yamekataa kuondoa vizuizi vya barabarani ambavyo vimekidhoofisha kisiwa hicho cha kanda ya Pasifiki ambacho ni himaya ya Ufaransa.

Ufaransa imewatuma wanajeshi takribani 1,000 katika kisiwa hicho kilichokumbwa na ghasia kwa wiki moja sasa, ambazo zimesababisha vifo vya watu sita, wakiwemo askari wawili na mamia kujeruhiwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hapo jana aliitisha mkutano mwingine wa dharura wa baraza lake la ulinzi na usalama na kusema kwamba kuna matumaini ya kurejea kwa hali ya utulivu.

Wakati huo huo Australia na New Zealand zimetangaza kwamba zitatuma ndege tatu kisiwani humo leo Jumanne ili kuwaokoa mamia ya watalii ambao wamekwama hotelini kufuatia ghasia zilizozuka.