Waandamanaji wakamatwa Zimbabwe
8 Novemba 2005Matangazo
Harare:
Polisi wa Zimbabwe wamewakamata watu 50 walipokuwa wanawazuia Watu kuandamana. Maandamano hayo yameitishwa na Chama kikubwa cha Wafanyakazi yakipinga kuzidi kwa umaskini na ufukara. Waandamanaji kadhaa walianza maandamano yao katikati ya mji mkuu, Harare, wakati polisi walipowavamia na kuwasomba katika makarandinga. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Zimbabwe (ZCTU), ambalo ni muungano wa vyama 30 vya Wafanyakazi, limewaomba Wanachama wake millioni moja kuandamana nchini kote leo kwa lengo la kuikumbusha serikali na Waajiri kuwa Wafanyakazi wana njaa, wamekasirika na wamechoka. Waziri wa Kazi na Huduma za Jamii, Nicholas Goche, amelaani maandamano hayo na kusema kuwa ni ya kisiasa.