1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vyaonya upungufu wa wafanyakazi wa umma Ujerumani.

14 Agosti 2023

Vyama viwili vya wafanyakazi nchini Ujerumani vimeonya juu ya kitisho cha upungufu wa watumishi kwenye sekta ya umma, unaoweza kusababisha matatizo makubwa katika uendeshaji wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4V7q9
Gewerkschaften zu Forderungen für die Tarifverhandlungen
Picha: Wolfgang Kumm/dpa/picture alliance

Gazeti la Bild am Sonntag limeripoti nafasi za kazi karibu 360,000 kwa sasa kwenye sekta hiyo nchini Ujerumani.Gazeti hilo limenukuu takwimu hizo kutoka taasisi ya ushauri ya McKinsey zinazoonyesha ifikapo mwaka 2030, huenda kukawa na upungufu wa watumishi karibu 840,000.Karibu watumishi milioni 1.3 wa sekta ya umma wanajiandaa kustaafu katika kipindi cha miaka saba ijayo, hii ikiwa ni kulingana na umoja wa watumishi wa umma, DBB.