1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya upinzani vyaitisha mgomo Ethiopia

8 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKY

Addis Ababa:

Vyama vya upinzani nchini Ethiopia, kufuatia machafuko yaliyotokea, vimetoa mwito wa kufanywa mgomo wa wiki moja nchini kote. Maduka mengi yamefungwa mjini Addis Ababa. Mashirika ya kimataifa yameiomba serikali ya Ethiopia kutotumia nguvu za kijeshi. Wapinzani wamekuwa wakilalamika kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi wa Mei mwaka huu na kudai kuwa umefanyiwa mizengwe. Viongozi 24 wa upinzani wamekamatwa na bado hawajafikishwa mahakamani.