1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya kisiasa vyakubaliana Gauck awe Rais wa Shirikisho

20 Februari 2012

Mada moja tu imehanikiza magazetini :uamuzi wa vyama vinavyounda serikali kuu ya muungano mjini Berlin kuridhia mteule wa vyama vya upinzani vya SPD/Die Grüne,Joachim Gauck awe rais wa shirikisho.

https://p.dw.com/p/145s3
Mgombea wa ridhaa wa wadhifa wa rais wa shirikisho Joachim GauckPicha: picture-alliance/dpa

Wengi wape, wanasema wahariri wakizungumzia jinsi kansela Angela Merkel alivyolazimika kuridhia shinikizo la mshirika wake mdogo serikalini FDP.Gazeti la Augsburger linaendelea kuandika:Kilikuwa chama cha FDP,kilichopelekea Angela Merkel aregeze kamba.Pengine tayari Angela Merkel alikuwa ameliorodhesha  pia jina la Joachim Gauck.Lakini lilikuwa shikinizo la chama cha FDP kumuunga mkono mteule wa vyama vya SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne,lililomzindua Angela Merkel atambue hatari ya kuweza kuvunjika serikali yake ya muungano na hivyo kumkubali Joachim Gauck.Kwa namna hiyo anaungama mwaka 2010 alifanya makosa .Hiyo ni aibu na pigo pia.Lakini pia ni ishara ya moyo wa ujasiri wa Angela Merkel.

Pressekonferenz im Bundeskanzleramt Bundespraesident
Kansela Angela Merkel (kulia)na Joachim GauckPicha: dapd

Gazeti la "Westdeutsche Zeitung linaandika:Inasikitisha kwamba jana serikali kuu ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na waliberali wa FDP imetoa picha mbaya.Ugonvi kuhusiana na Gauck ulitishia kuitia kishindo kikubwa serikali kuu ya muungano.Kwasababu kinyume na CDU/CSU,waliberali wao waliusikia mwito wa umma na kufungamanisha hatima ya serikali ya muungano na jina la Gauck.Mwenyekiti wa chama kilichopwaya cha FDP,Philipp Rössler alitumia turufu yake ya mwisho na kushinda.Kwakua amemng'ang'ania Gauck anawaeza hivi sasa kujinata kama mwenyekiti mstahiki.Suala lakini ni kama hali hiyo itawasaidia waliberali katika uchaguzi ujao katika jimbo la Schleswig-Holstein-Jibu tusibiri ntuone.

Gazeti la Badische Neueste Nachrichten linaandika:Kansela Angela Merkel amelazimika kufanya marekebisho.Uamuzi wa jana usiku wa vyama ndugu vya CDU/CSU kuridhia Joachim Gauck achaguliwe kuwa rais wa shirikisho,ni mbinu ambazo hazikuwa rahisi kuzifuata.Wote wataondoka na ushindi wakianzia SPD na walinzi wa mazingira ambao tangu miaka miwili iliyopita walishauri Gauck achaguliwe kuwa rais wa shirikisho.Na FDP pia kwasababu  jana waligonga ndipo na kufanikiwa.Na pia CDU ambao hawatakawia kutambua kwamba wana mafungamano makubwa zaidi na rais huyo kuliko vile walivyofikiria.

Der Präsidentschaftskandidat Joachim Gauck
Atakaekuwa rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Joachim GauckPicha: picture-alliance/dpa

Gazeti la mjini Bonn,General Anzeiger linahisi uamuzi wa walio wengi  ndio uliomfanya kansela Angela Merkel aregeze kamba.Gazeti linaendelea kuandika:Kura za walio wengi ndizo zilizomfanya kansela Angela Merkel afanye marekebisho.Matokeo yake ni kwamba Ujerumani kwa mara ya kwanza itakuwa na rais wa shirikisho ambae jamii hawatakuwa na shida nae hata kidogo.Kwamba yeye sawa na Angela Merkel ni waprotestanti na wametokea sehemu ya mashariki,watakaokereka na hali hiyo ni wale tu wanaodai pawepo wezani.Na Angela Merkel je?Ameshindwa na atabidi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 atafute mshirika mwengine-lakini na hilo pia lina faida yake.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman