1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zazuka Albania

22 Januari 2011

Polisi wajaribu kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali ya waziri mkuu Sali Berisha. Waandamanaji hao wanataka serikali ijiuzulu kutokana na madai ya rushwa.

https://p.dw.com/p/100s0
Magari kadhaa ya polisi yaliwashwa moto katika vurugu hizoPicha: DW/Muka

Watu watatu walipigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Albania Tirana hapo jana, wakati waandamanaji walipokabiliana na polisi katika mkutano wa upinzani dhidi ya serikali. Waziri mkuu Sali Berisha amewataja waandamanaji hao kuwa jaribio la upinzani kuanza machafuko yalio mfano wa Tunisia. Chama cha upinzani cha kisoshalisti kimekataa kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2009 ambapo chama cha waziri mkuu Berisha kilishinda kwa tafauti ya kura chache tu. Vurugu hizo zilizuka wakati waandamanji walipokusanyika nje ya ofisi ya waziri huyo mkuu,wakiitaka serikali yake ya kihafidhina ijiuzulu kutokana na madai ya rushwa. Magari kadhaa ya polisi yaliwashwa moto na waandamanaji waliwarushia polisi mawe na vigongo, wakilishambulia pia jengo hilo. Polisi walijibu kwa kutumia hewa ya kutoa machozi, mipira ya maji, na risasi za mpira kujaribu kuwatawanya waandamanaji hao.

Tirana Albanien Protest
Picha: DW/Muka
Albanien Ministerpräsident Sali Berisha
Waziri mkuu Sali Berisha.Picha: Mimoza Dhima

Mwandishi: Maryam Abdalla/Afp/Rtre
Mhariri: Abdul-Rahman.