Ghasia zimeendelea kushuhudiwa katika miji kadhaa ya Senegal ukiwemo Dakar kufuatia hukumu ya miaka miwili jela dhidi ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko. Watu wasiopungua tisa wameripotiwa kuuawa tangu machafuko yalipoanza. Lilian Mtono amezungumza na mwandishi wa habari Chrispin Mwakideu aliyeko kanda ya Afrika Magharibi na anayefuatilia kwa karibu matukio hayo. Anatujuza hali ilivyo.