1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto nyingi kwa Rais Muhammadu Buhari

1 Desemba 2015

Baada ya kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la Biafra nchini Nigeria yaliyosababisha vifo vya watu milioni moja, vuguvugu kusini mashariki mwa nchi hiyo linataka jimbo la Biafra lijitawale.

https://p.dw.com/p/1HFVO
Nigeria Muhammadu Buhari Präsident Rede vor der UN Vollversammlung
Picha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Miito kama hii imekuwa ya mara kwa mara tangu kiongozi wa kundi hilo ambalo Ikedi anawakilisha katika eneo la Enugu ulio mji mkuu wa eneo hilo alipokamatwa mwezi Octoba,na kusababisha maelfu ya watu katika eneo linalozalisha mafuta kwa wingi la kusini Mashariki kujiunga na maandamano hayo katika wiki za hivi karibuni wakitaka aachiliwe huru.

Hii ni changamoto nyingine kwa Rais Muhammadu Buhari ambaye anakabiliana na kushuka kwa uchumi katika taifa hilo ,kundi la itikadi kali la Boko Haram kaskazini mashariki na hofu ya kurejea kwa shughuli za kijeshi katika eneo tajiri kwa mafuta la Delta Kusini wakati muda wa mwisho utakapomalizika mwezi Disemba.

Kama ilivyo kwa wengi katika vuguvugu la wanaotaka kujitenga katika eneo la kusini mashariki,Ikedi alizaliwa muda murefu baada ya kumalizika kwa vita vya Biafra.

Bila kuwa na chochote kitakachoashiria anaunga mkono kujitenga kwa Biafra kama vile bendera au fulana,ili kuepuka kuwavutia polisi, amesema umaskini na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira katika eneo hilo ni ishara ya kutelekezwa na serikali.

"Wanataka kutufanya masikini .Wanaamini njia ya pekee kututawala ni kuendelelea kututaabisha"Ikedi amesema kwa sauti ya kutetemeka huku akisema kundi lake la watu asili wa Biafra (IPOB) wanataka kura ya maoni.

Wanalalamika eneo lao limetelekezwa

Kundi hilo linaelezea matatizo yanayowafanya watake jimbo la Biafra liwe huru, swala ambalo msemaji wa rais Buhari, Garba Shehu alikataa kuzungumzia akiongeza kuwa hana ufahamu kuwa serikali inafanya chochote kuhusu swala hilo.

Symbolbild Nigeria Straße
Barabara katika jimbo la Biafra nchini NigeriaPicha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Barabara kuu zinazounganisha miji ya kusini mashariki zinavunja moyo wafanyabiashara katika eneo hilo ambao wanasema barabara hizo ambazo hazijawekwa lami kikamilifu,zina mashimo, zinastahili kuwa kichocheo cha biashara lakini sasa ni hatari kuzitumia.

Taka iliyopembeni mwa barabara,pamoja na harufu mbaya kutoka kwa mfumo wa maji machafu usiofunikwa inaelezea kutengwa kwa miaka 45 tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mapigano ya 1967-70 yalifuatwa na jaribio la kujitenga la watu wa Igbo mashariki.Wengi wa watu milioni moja walipoteza maisha yao kutokana na njaa na maradhi na wala si vita.

Kama wakati huo kwa sasa,Watu wa Igbo wanasema wametengwa kutoka nyadhifa za serikali na kunyimwa ufadhili muhimu wa kustawisha muundombinu,shule na hospitali.

Kiongozi wa jamii ya watu wa Igbo wa Biafra Nnamdi Kanu mwanaharakati ambaye anatumia muda wake huko Uingereza na Nigeria kwa kueneza mawazo yake kwenye mitandao ya kijamii na Radio Biafra alikamatwa mwezi uliopita kwa mashtaka ya uhalifu na kwa kuwa mwanachama wa kundi lisilo halali.

Mchambuzi wa maswala ya kisiasa Oreke Chukwunolye amesema uamuzi wa kumkamata Kanu,ambaye hakuwa maarufu ingawa ufuasi wake kwenye mtandao wa kijamii unashinda uugwaji wake mkono sehemu za mashinani,ni kosa kwani kukamatwa kwake kunamuongezea umaarufu na kumfanya atambulike zaidi.

Bado kungali hali ya taharuki.Wanaoendeleza kampeni za IPOB wanasema wamejitolea kufanya maandamano ya amani,lakini maandamano yao yalisababisha jeshi la nchi hiyo kutoa onyo kwamba juhudi zozote za kugawanya nchi hiyo,zitapingwa vikali.

Mwandishi:Bernard Maranga/Reuters

Mhariri: Daniel Gakuba