Von der Leyen kuwania ukuu wa NATO
1 Aprili 2023Matangazo
Haya yameripotiwa jana na gazeti la The Sun lililonukuu duru za kidiplomasia.
Ripoti ya gazeti hilo la The Sun likinukuu vyanzo vya Uingereza, imesema kuwa Uingereza huenda ikapinga kuchaguliwa kwa von der Leyen ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa ulinzi wa Ujerumani na kutaja rekodi yake mbaya ya usimamizi wa jeshi la nchi hiyo.
Soma zaidi: NATO, EU zaapa uungaji mkono zaidi kwa Ukraine
Gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag pia limeripoti kuwa Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez na Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ni miongoni mwa wawaniaji wanaoongoza kumrithi mkuu wa sasa wa NATO, Jens Stoltenberg, ambaye muda wake wa uongozi unafikia kikomo mwezi Oktoba baada ya kuhudumu kwa takriban miaka tisa.