Von der Leyen apendekeza kuundwa kwa bodi ya akili bandia
10 Septemba 2023Matangazo
Akizungumza mwishoni mwa mkutano wa G20, Von der Leyen amependekeza kuundwa kwa bodi sawa na Jopo la Kiserikali la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC), ambayo inaweza kukabiliana na athaari kwa kijamii, na faida za teknolojia.
Soma pia: Teknolojia ya Akili bandia huenda ikasababisha ubaguzi
Athari za akili bandia, zimekuwa mjadala mkali duniani kote katika miezi kadhaa hasa badaa ya Programu za ChatGPt na Bard ambazo zinaweza kutengeneza picha kulingana na maelezo ya maandishi kuibua wasiwasi kwamba zinaweza kutengeneza na kueneza habari potofu.