Kasi ya ujenzi na kuimarisha miundombinu na makaazi ya watu inazidi kuongezeka visiwani Zanzibar hadi kusababisha upungufu wa mchanga. Makala ya Mtu na Mazingira inatizama athari za kiafya na kimazingira zitokanazo na viwanda vya utengenezaji matofali vinavyotumia vumbi badala ya mchanga. Msimulizi ni Salma Said.