Vitisho vyachelewesha uundwaji Baraza la rais Haiti
26 Machi 2024Maafisa nchini Haiti wanasema msukosuko mwengine unaolihusisha baraza la rais litakalokuwa na jukumu la kumchagua kiongozi mpya wa nchi hiyo, umepelekea kufanyika kwa mikutano kadhaa ya viongozi wa Caribbean na maafisa kutoka Marekani, Canada na Ufaransa.
Soma pia: Jukumu la kihistoria la Ufaransa katika mzozo wa Haiti
Kulingana na afisa mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba, baraza hilo bado halijaapishwa kutokana na hofu inayowakabili wanachama wake, miongoni mwa mambo mengine.
Kucheleweshwa kuanzishwa kwa baraza hilo kunatokana na mashambulizi yanayofanywa na magenge kote katika mji mkuu wa haiti.
Soma pia:Ufaransa kuwaondoa raia wake Haiti kufuatia machafuko
Tangu Februari 29, watu waliojihami kwa bunduki wameviteketeza vituo vya polisi, kuushambuliwa uwanja mkuu wa ndege na kuupelekea kufungwa hadi sasa na kuyavamia magereza mawili makuu na kuwaachia huru zaidi ya wafungwa 4,000.