Vita vya Sudan vyaingia mwezi mmoja bila dalili ya kuisha
15 Mei 2023Matangazo
Mapigano hayo yanaendelea licha ya mazungumzo kati ya pande mbili za jeshi yanayofanyika nchini Saudi Arabia.
Jiji la Khartoum na miji inayopakana na mji huo mkuu ya Bahri na Omdurman iliyo kwenye mto Nile ndiyo miji inayokabiliwa na mapigano makali tangu pande mbili za jeshi zilipoanza kupigana mnamo tarehe 15 mwezi uliopita.
Mashambulizi yaendelea Khartoum wakati wapinzani wakikutana Saudia
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa mapigano hayo yamesababisha vifo vya takriban watu 676 na wengine 5,576 wamejeruhiwa japo bado ziko ripoti za watu kupotea. Idadi kamili ya vifo hivyo inatarajiwa kuwa juu zaidi tofauti na iliyoripotiwa.
Jimbo la magharibi la Darfur ni miongoni mwa maeneo yanayokumbwa na mapiganio hayo ya nchini Sudan.