1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Vita vya miezi sita vimeua watu 9,000 nchini Sudan

16 Oktoba 2023

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, amesema vita vya Sudan ambavyo vimedumu kwa miezi sita sasa, vimewaua hadi watu 9,000.

https://p.dw.com/p/4XZBC
Martin Griffiths, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa.
Martin Griffiths, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa.Picha: Martial Trezzini/dpa/Keystone/picture alliance

Griffiths alisema hayo jana Jumapili, na kueleza zaidi kuwa vita hivyo kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF), vimesababisha moja kati ya migogoro mibaya ya kibinadamu katika historia ya hivi karibuni

Sudan, imezongwa na machafuko tangu katikati ya mwezi Aprili, wakati mvutano kati ya mkuu wa majeshi Jenerali Abdel-Fattah Burhan na kamanda wa kikosi cha RSF Jenerali Mohamed hamdan Dagalo, ulipogeuka vita vya wazi.

Kulingana na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni 4.5 wamekuwa wahamiaji wa ndani nchini Sudan, huku wengine zaidi ya milioni 1.2 wakikimbilia nchi jirani.

Griffiths amesema pia kuwa mapigano hayo yamewaacha watu milioni 25, hiyo ikiwa zaidi ya nusu ya idadi jumla ya Wasudan wanaohitaji misaada ya kibinadamu.