1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya kupambana na umaskini:

19 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLm

Umoja wa Mataifa:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amesema kuwa nchi zinazoendelea na Wafadhili lazima zishirikiane kwa dhati katika kupambana na umaskini na utekelezaji wa malengo ya maendeleo kabla ya mkutano mkuu wa Viongozi wa Umoja wa Mataifa utakaofanywa mwezi wa Septemba mwaka huu. Bw. Annan amesema kuwa nchi zinazoendelea lazima ziunganishe rasili mali zao zote katika kupambana na umaskini. Amerudia mwito wake kwa nchi fadhili kuongeza misaada yao na kufikia kiwango cha asili mia 0.7 cha pato zima la taifa hadi kufikia mwaka 2015. Hilo ni lengo mojawapo kati ya malengo kadhaa ya Maendeleo ya Milenia yaliyoidhinishwa na Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Bw. Annan amesema hayo wakati alipohutubia mkutano wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa, Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF), Benki Kuu ya Dunia, Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa.