Tangu 2015, wanawake 20,000 wa Nigeria wamekuwa waathiriwa wa usafirishaji haramu wa watu. Mji wa Benin ambao ni makao makuu ya mkoa huo umekuwa kitovu cha uhalifu huo. Sasa maafisa wanataka kuuangamiza mtandao huo wa usafirishaji wa watu. Mwandishi wa habari wa DW katika makala ya Vijana Mubashara Jan-Phillip Scholz aliandamana nao