Wimbi la karibuni la utekaji nyara, vifo na watu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha vimezusha hofu miongoni mwa Watanzania na kuzusha tuhuma kwamba kuna kikosi cha siri cha kikatili chenye kutenda hayo. Mwenendo huo umezidi kuiweka katika hali ya taharuki Tanzania baada ya kutekwa nyara mwanamuziki Ibrahim Musa kwa jina la usanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu.