1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Viongozi wawasili kwa ajili ya Mkutano wa Baraza Kuu la UN

23 Septemba 2024

Mamia ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamewasili mjini New York, Marekani kuhudhuria Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4kzAh
Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wakuu na viongozi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuanzia Jumanne Septemba 24, 2024Picha: Lokman Vural Elibol/AA/picture alliance

Viongozi hao ambao ni marais, manaibu rais, wanamfalme na mawaziri wanatarajiwa kutoa hotuba zao kuanzia hapo kesho na kwa muda wa siku sita.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: "Kutomwacha mtu nyuma, kuchukua hatua kwa pamoja kwa ajili ya kuendeleza amani, maendeleo endelevu na heshima ya ubinadamu kwa vizazi vya sasa na vijavyo."

Yanayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo wa UNGA ni pamoja na matatizo yanayoukabili ulimwengu hasa vita vya Mashariki ya Kati na huko Ukraine na pia migogoro ya hali ya hewa, huku baadhi ya viongozi hasa wale wa Afrika wakitarajiwa kushinikiza mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.