Viongozi walioshitakiwa
Rushwa, ufisadi ama matumizi mabaya ya madaraka: DW inawaangazia viongozi maarufu duniani waliowahi kushitakiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Luiz Inacio Lula da Silva, Brazil
Lula alipatikana na hatia ya ufisadi na kutakatisha fedha baada ya kuhusishwa katika kashfa ya "Car Wash", mashitaka ya ufisadi ambayo ni makubwa zaidi yaliyofichua kuenea kwa rushwa miongoni mwa wasomi nchini Brazil. Lula, ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 2003 na 2010, alihukumiwa kifungo cha miaka 9.5 jela. Bado ana nafasi ya kuikata rufaa ya hukumu hiyo.
Cristina Fernandez, Argentina
Cristina Fernandez, ambaye aliwahi kuwa mke wa rais na baadae rais nchini Argentina kati ya mwaka 2007 hadi 2015, alihukumiwa kwa mashtaka ya rushwa mwaka 2016. Alidaiwa kutoa kwa upendeleo mikataba ya ujenzi ya umma. Alikataa kufanya kosa lolote. Fernandez sasa anataka kurudi kisiasa, hatua ambayo baadhi ya wafuatiliaji wanasema ni jitihada za kutafuta kinga dhidi ya mashtaka hayo.
Park Geun-hye, South Korea
Kufuatia miito ya umma iliyodumu miezi kadhaa juu ya wimbi la madai ya rushwa, Rais wa kwanza wa kike wa Korea Kusini Park Geun-hye hatimaye aliondolewa mamlakani. Alishtakiwa kwa ulafi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Park alipigiwa kura ya kutokuwa na imani nae mwezi Disemba mwaka 2016.
Ehud Olmert, Israel
Olmert mwenye umri wa miaka 71, aliyekuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2006 na 2009, alihukumiwa kwa rushwa mwaka 2014. Alianza kutumikia kifungo Februari 2016 lakini aliachiliwa mapema Julai 2017 baada ya hukumu yake kufupishwa. Alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa zamani wa Israeli kwenda jela. Benjamin Netanyahu akawa mrithi wake.
Adrian Nastase, Romania
Adrian Nastase alishtakiwa kwa madai ya rushwa mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili. Wakati ambapo hukumu hiyo kutajwa, alikuwa ndiye mkuu pekee wa serikali aliyehukumiwa kifungo cha kufungwa gerezani baada ya miaka 23 kufuatia Mapinduzi ya Kiromania. Alikuwa waziri mkuu wa Romania kati ya mwaka 2004-2006.
Charles G. Taylor, Liberia
Charles Taylor alihukumiwa miaka 50 gerezani mwaka 2012 kutokana na nafasi yake kwenye mauaji ya kiholela yaliyofanywa nchini Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990. Taylor alikuwa rais wa zamani wa kwanza aliyehukumiwa na mahakama ya kimataifa ya kimbari tangu mashitaka ya Nuremberg huko Ujerumani baada ya Vita Kuu ya II. Alikuwa rais wa Liberia tangu 1997-2003.