1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Urusi na China wakutana Moscow

21 Agosti 2024

Ikulu ya Urusi imesema Rais Vladmir Putin leo amekutana na Waziri Mkuu wa China, Li Qiang mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4jkQu
Rais wa Urusi, Wladimir Putin, akimsalimia Waziri Mkuu wa China, Li Qiang.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, kushoto, na Waziri Mkuu wa China Li Qiang wakipeana mikono wakati wa mkutano wao kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Urusi, Agosti 21, 2024.Picha: Alexey Filippov/Sputnik/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la serikali RIA, limemnukuu Rais Putin akisema kuwa nchi hizo zina mipango mikubwa ya pamoja, miradi katika maeneo ya kiuchumi na kiutu, na wanatarajia itadumu kwa miaka mingi. Mapema, Li alisema kuwa China iko tayari kufanya kazi na Urusi ili kuimarisha ushirikiano wa miradi wa pande zote. Li amekutana pia na Waziri Mkuu wa Urusi Mikhail Mishustin, ambapo wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa karibu katika sekta ya nishati. Mishustin amemueleza mgeni wake kwamba Urusi iko tayari kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta ghafi kwa China. China inavichukulia vita vya Urusi nchini Ukraine kama vinavyovuruga utaratibu wa kimataifa, ingawa iko upande wa Urusi katika suala hilo.