Kansela wa Ujerumani ziarani Tokyo
18 Machi 2023Matangazo
Wawili hao wanajadili ushirikiano wa karibu wa kiuchumi kati ya nchi zao. Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita kwenye ushirikiano wa kimataifa wakati Ujerumani ikitafuta kupunguza utegemezi wa kiuchumi kwa malighafi za China.
Soma zaidi Ujerumani yajizatiti kusaka malighafi za viwanda vyake
Mwaka uliopita, Japan ambayo pia ni mnunuaji mkubwa wa malighafi, ilipitisha sheria makhsusi ya usalama wa kiuchumi. Sheria hiyo inatazamwa na serikali yaUjerumani kuwa mfano wa kuigwa.
Katika mkutano huo, Kansela wa Ujerumani ameambatana na mawaziri wake wakiwemo waziri wa uchumi Robert Habeck, Waziri wa mambo ya kigeni Annalena Baerbock na waziri wa fedha Christian Lindner. Mazungumzo ya Scholz na Kishida, yanatazamiwa pia kuangazia masuala ya usalama.