Viongozi wa nchi za Kiarabu kukutana Misri
19 Januari 2011Wakati huo huo, Rais wa Tunisia, Foued Mebazaa na Waziri Mkuu, Mohammed Ghannouchi jana wamejiuzulu kwenye chama tawala katika hatua ya kutimiza matakwa ya wanasiasa wa upinzani na viongozi wa chama kikuu cha wafanyakazi.
Kituo cha televisheni ya taifa kimeripoti kuwa viongozi hao wamebakia katika nafasi zao kama rais na waziri mkuu. Mapema, mawaziri wanne walijiuzulu kutoka katika serikali ya mpito ya Waziri Mkuu Ghannouchi. Wizara muhimu zinaendelea kushikiliwa na wafuasi wa rais wa zamani, Ben Ali.
Utawala wake wa miaka 23 ulimalizika baada ya wiki kadhaa za maandamano kupinga viwango vya umasikini na ukosefu wa ajira nchini humo. Kwenye mji mkuu wa Tunis, jana polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao wanataka kuvunjwa kwa chama tawala.