NATO yajadili kuimarisha utengenezaji silaha Ukraine
26 Novemba 2024Mawaziri wa Ulinzi kutoka Ujerumani, Ufaransa, Poland, Italia na Uingereza wanakutana mjini Berlin kujadili hatua za kuimarisha ulinzi na usalama barani Ulaya.
Soma zaidi: Nchi za NATO zapania kuimarisha utengenezaji silaha Ukraine
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema kipaumbele ni kuunda na kununua droni zinazoendeshwa na akili mnemba pamoja na kushirikiana na nchi zingine za NATO kuongeza uzalishaji wa silaha.
Aidha mawaziri hao wamejadili pia kuhusu Urusi kurusha kombora la masafa marefu katika eneo la Dnipro ambalo Rais Vladimir Putin alisema lilikuwa jaribio la kombora lake jipya la Oreshnik.
Putin alionya kwamba Moscow inahisi kuwa ina "haki" ya kushambulia vituo vya kijeshi katika nchi zinazoruhusu Ukraine kutumia silaha zao dhidi ya Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikosoa hatua ya Urusi na akaomba mifumo mipya ya ulinzi wa anga ili kukabiliana na tishio hilo jipya.