1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa kijeshi wa Niger wamkosoa Guterres

23 Septemba 2023

Viongozi wa kijeshi wa Niger wamekosoa kile walichokiita "vitendo vya upotofu" vya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa madai ya kuwazua wasishiriki mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4Wixj
 Assimi Goïta, Abdourahamane Tiani, Ibrahim Traoré
Picha: Francis Kokoroko/REUTERS; ORTN - Télé Sahel/AFP/Getty; Mikhail Metzel/TASS/picture alliance

Viongozi wa kijeshi waliompindua rais wa Niger wamekosoa kile walichokiita "vitendo vya upotofu" vya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, wakimtuhumu kwa kuzuia ushiriki wao katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja huo.Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya umma, jeshi lilitoa wito kwa "wananchi na jumuiya kimataifa kushuhudia vitendo vya Guterres" ambavyo limedai vinaweza kudhoofisha juhudi zozote za kumaliza mgogoro katika taifa lao.Taarifa hiyo iliongeza kuwa katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa "alipotoka kwa kuzuia ushiriki kamili wa Niger katika kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa".Tangu mapinduzi ya Julai 26, rais aliyepinduliwa na jeshi, Mohamed Bazoum, mkewe na mtoto wao wamezuliwa katika kizuizi cha nyumbani.