Viongozi wa kidini wazindua kampeni ya amani mashariki Kongo
14 Machi 2023Vyanzo kutoka mashirika ya kiraia katika maeneo mbalimbali wilayani Masisi, vimehakikisha taarifa ya kuanza kuondoka kwa waasi hao wa M23 katika mji mdogo wa Mweso, Kiuli, Malehe na kwenye milima inayoinukia kijiji cha Karuba ambako misururu ya wapiganaji hao ulionekana wote wakiwa wamebeba mizigo na silaha lakini bila kueleza ni wapi walielekea, kama anavyoshuhudia mkaazi huyu wa kitshanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Soma pia: Usalama wazidi kuzorota nchini Kongo
Hata hivyo, upande wa mashirika ya kiraia wamesema kuwa na mashaka kufuatia hatua hiyo ya M23 kwa kile wanachotaja kama ujanja wa kuendelea kuvishikilia vijiji vingine
Wakati huo huo, katika mkutano wao na vyombo vya habari ,viongozi wa madhehebu mbalimbali mkoani kivu kaskazini walikutana hiyo jana hapa mjini ambapo walijadili hali jumla ya usalama mkoani Kivu kaskazini ambako Wakuu hao kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini wamewataka wananchi kukuza amani ambayo ni njia pekee ya kuzima mzozo unaoendelea kufukuta kati ya serikali na kundi la waasi wa M23
Soma pia: M23 wakabiliana na jeshi na kukaidi amri ya kusitisha mapigano Kongo
Haya yanajiri siku moja baada ya ziara ya siku 3 ya wajumbe wa baraza la umoja wa mataifa hapa nchini Congo ,waliolitaka kundi hilo la waasi wa M23 kuondoka na kuyaacha maeneo yote linalodhibiti.