1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 katika mbinyo kutimiza malengo

16 Novemba 2014

Australia imetoa wito wa dakika za mwisho leo(16.11.2014)kwa viongozi wa G20 kutumia uwezo wao wote wa sera kuurekebisha uchumi wa dunia na kuchochea ufanisi, na kufikia lengo la kuongeza ukuaji kwa asilimia mbili.

https://p.dw.com/p/1DoE5
G20-Gipfel in Brisbane Familienfoto 15.11.2014
Viongozi wa G20 katika picha ya pamoja mjini BrisbanePicha: Andrew Taylor/G20 Australia via Getty Images

Mataifa makubwa yenye viwanda yameapa kuongeza ukuaji wa uchumi wao kwa pamoja kwa dola trilioni mbili juu ya kiwango cha sasa kilichotabiriwa katika miaka mitano ijayo, kupitia mageuzi ya sera za ndani.

Lengo la ukuaji wa uchumi duniani

Wazo katika mkutano wa viongozi wa G20 nchini Australia limekuwa kuangalia itakuwaje , ambapo mchakato huo unatarajiwa kutangazwa baadaye leo Jumapili(16.11.2014) katika kile kinachojulikana kama "Mpango wa kuchukua hatua wa Brisbane".

G20 Gipfel Barack Obama und Tony Abbot 15.11.2014
Rais barack Obama na waziri mkuu wa Australia Tony AbbottPicha: Reuters

"Ukweli ni kwamba lengo la asilimia mbili ambalo lilitangazwa mjini Sydney mwaka huu limefikiwa, lakini litaendelea," waziri wa hazina wa Australia Joe Hockey ameimbia televisheni ya taifa. "Hatuwezi kubweteka. Dunia inahitaji ukuaji."

Jana Jumamosi (15.11.2014) rais Barack Obama ameweka wazi kwamba Marekani haiwezi "kuubeba uchumi wa dunia", na kwamba mataifa mengine ya G20 yanapaswa kufanya juhudi zaidi kuongeza ukuaji na kuunda nafasi za kazi.

Ikichagizwa na ukosefu wa kazi katika kiwango chake cha chini kabisa tangu Julai mwaka 2008 , uchumi wa Marekani unapata nguvu katika wakati maeneo mengine ya nguvu za uchumi wa dunia , hususan Ulaya na Japan , yanaanza kuzorota.

Jean-Claude Juncker erste Sitzung der neuen EU Kommission 05.11.2014 Brüssel
Jean-Claude Juncker rais mpya wa halmashauri ya Umoja wa UlayaPicha: Reuters/F. Lenoir

"Kwa hiyo hapa Brisbane kundi la G20 linawajibu wa kuchukua hatua, kuimarisha mahitaji na uwekezaji zaidi katika miundo mbinu na kuunda nafasi za ajira kwa watu wote wa mataifa yetu," amesema rais wa Marekani Barack Obama.

Ulaya yahitaji kukuza uchumi wao

Hockey amesema kupiga hatua kupindukia lengo la asilimia mbili inawezekana iwapo viongozi wa Umoja wa Ulaya wataanza kuingiza mabilioni ya dola katika uchumi wa eneo la sarafu ya euro ambao unasinzia.

Mkuu mpya wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker hapo kabla ameainisha ajenda ya mageuzi, ikiwa ni pamoja na mpango wa euro bilioni 300 wa uwekezaji kuinua ukuaji wa uchumi, nafasi za ajira na ushindani.

Maelezo halisi ya utaratibu huo bado hayajatolewa. Waziri wa fedha ameongeza kuwa viongozi wa kundi la G20 hawataachwa huru inapokuja katika suala la kutimiza ahadi zao za kuondoa ukiritimba na kuhimiza uwekezaji katika miundo mbinu kutoka kwa watu binafsi ili kuchochea ukuaji.

BRICS am Rande des G20-Gipfel in Brisbane 15.11.2014 Dilma Rousseff
Viongozi wa mataifa yanayoinukia kiuchumi BRICSPicha: picture-alliance/dpa/Druzhinin Alexei

"Kile tulichokifanya ni kwamba tumelipa nafasi shirika la fedha la kimataifa IMF na benki kuu ya dunia kuangalia na kuripoti kwetu kuhusu utendaji wa nchi moja moja, " amesema.

Australia ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo imefanyakazi kwa bidii kuweka mtazamo wa kundi la G20 mwaka huu kuhusu suala la uchumi , ikiwa ni pamoja na kupambana na ukwepaji wa kulipa kodi duniani.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani