1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi wa China waahidi msaada zaidi kuchochea uchumi

Josephat Charo
30 Julai 2024

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamesisitiza umuhimu wa mageuzi zaidi kuimarisha shughuli za kiuchumi na sekta ya mali ya nchi hiyo inayosuasua.

https://p.dw.com/p/4itrn
Giorgia Meloni atembelea China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria ufunguzi wa mkutano wa saba wwafanyabiashara wa China na Italia pamoja na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni huko Beijing, mji mkuu wa China, Julai 28, 2024.Picha: Yue Yuewei/Xinhua/IMAGO

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la taifa kufuatia mkutano uliojikita katika kuimarisha ukuaji uchumi. China iko mbioni kufikia lengo lake la ukuaji uchumi kwa aslimia tano mwaka huu, kiwango kinachoelezwa na wataalamu kuwa kikubwa mno, huku taifa hilo lenye uchumi wa pili kwa ukubwa ulimwenguni likikabiliwa na changamoto zikiwemo soko la mali zisizohamishika lenye madeni, matumizi yaliyoongezeka na ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana. Mkutano wa leo wa maafisa wa vyeo vya juu wa chama cha Kikomunisti ni fursa kwa uongozi wa juu wa chama kutathmini hali ya sasa ya uchumi na kuweka mueleke mpya wa sera kwa nusu ya pili ya mwaka.