Viongozi wa Afrika walalamikia mfumo wa fedha kimataifa
30 Mei 2024Miito ya namna hiyo imekuwa ikiongezeka miaka ya karibuni katika wakati nchi kadhaa za kiafrika zinaandamwa na viwango vikubwa vya madeni ya mikopo iliyochukuliwa kufadhili miradi ya maendeleo.
Wakizungumza mjini Naironbi kwenye mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB viongozi wa mataifa ya bara hilo wamesema ili "kuibadilisha Afrika" ni lazima nchi za bara hilo zipate nafasi ya kuifikia mitaji na fedha kwenye mfumo wa kimataifa.
Soma pia:WFP inahitaji dola milioni 400 kuwalisha mamilioni ya watu wanaohitaji msaada Barani Afrika
Hata hivyo mwenyeji wa mkutano huo, Rais William Ruto wa Kenya amesema Afrika inakabiliwa na vizingiti kutokana na mfumo wa sasa kifedha wa kimataifa ambao unayalazimisha mataifa ya bara hilo kupata fedha kwa viwango vya riba.
Amesema baadhi ya viwango vya riba ya mikopo vinapindukia mara 8 hadi 10 ya vile vinavyotolewa kwa nchi nyingine.