Viongozi wa Afrika walaani mashambulizi ya Israel huko Gaza
17 Februari 2024Katika ufunguzi wa mkutano huo Rais wa Halmashauri ya Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema, mashambulizi ya Israel ni "ukiukwaji wa wazi" wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kuishutumu Israel kwa "kuwaangamiza" wakaazi wa Gaza.
Faki alimuhakikishia Waziri Mkuu wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mohammad Shtayyeh ambae amehudhuria mkutano huo kuwa wanaonesha mshikamano na watu wa Palestina kutokana na kile alichokisema "mashambulizi ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya wanadamu."
Aidha Faki amezungumzia wasiwasi wa kuzuka upya kwa mapinduzi ya kijeshi barani humo, huku akigusia mizozo ikiwemo mkwamo wa kisiasa nchini Senegala, ghasia mashiri mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ametoa wito wa mshikamano ili kukabiliana na changamoto katika bara hilo lenye watu takriban bilioni 1.3.