Mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Afrika umekamilika hapo jana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, azimio muhimu lililofikiwa likiwa kuhakikisha nchi za bara la Afrika ziunde sera za kuwawezesha wakimbizi na watu waliolazimika kuyahama makazi yao, wapate maisha bora na huduma bora katika nchi ambazo wanaishi.