1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi kutia saini makubaliano ya DRC

24 Februari 2013

Marais kutoka mataifa ya eneo la maziwa makuu barani Afrika wanakutana Jumapili(24.02.2013)katika juhudi za kufikia makubaliano yenye lengo la kupatanisha katika eneo mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

https://p.dw.com/p/17ko5
U.N. Secretary-General Ban Ki-moon arrives for the 18th African Union (AU) Summit in the Ethiopia's capital Addis Ababa, January 29, 2012. REUTERS/Noor Khamis (ETHIOPIA - Tags: POLITICS ENERGY)
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ataongoza utiaji sainiPicha: Reuters

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewaalika marais 11 katika tukio hilo la kutiwa saini kwa kile kinachojulikana kama makubaliano ya mfumo wa amani, ikiwa ni juhudi za kufikisha mwisho mzozo huo, lakini bila kuwa na maelezo maalum. Makubaliano hayo yatatiwa saini katika makao makuu ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Iwapo yatafanikiwa makubaliano hayo yanaweza kusababisha kuundwa kwa kikosi maalum cha jeshi la umoja wa mataifa kitakachoweza kuingilia kati , katika eneo la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kupambana na waasi pamoja na juhudi mpya za kisiasa.

In this Wednesday Nov. 21, 2012 photo released by Uganda's Presidential Press Services, Uganda's President Yoweri Museveni, center, sits with his counterparts Paul Kagame of Rwanda, left, and Joseph Kabila of Congo during a meeting in Kampala, Uganda. The three heads of the states want the M23 rebels out of Goma, a town they captured from Congo army. (Foto:Presidential Press Services/AP/dapd)
Mkutano baina ya viongozi wa Uganda, rwanda na CongoPicha: dapd

Viongozi waalikwa

Msemaji wa umoja wa mataifa Martin Nesirky amesema kuwa viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Angola, Burundi, jamhuri ya Afrika ya kati , Jamhuri ya Congo, Rwanda, Afrika kusini , Sudan ya kusini, Tanzania, Uganda na Zambia wamealikwa.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika , mataifa 11 ya mkutano wa kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu , (ICGLR) pamoja na jumuiya ya wanachama 14 ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, watakuwa "wadhamini wenza", amesema Nesirky. Juhudi za hapo awali za kufitiwa saini kwa makubaliano hayo mwezi uliopita zilisitishwa katika dakika za mwisho.

epa03084113 A handout image made available by the South African Government Communication and Information System (GCIS) shows a general view of the the new African Union building where the present 26th meeting of the NEPAD Heads of State and Government Orientation Committee (HSGOC) is being held, Addis Ababa, Ethiopia, 29 January 2012. EPA/Jacoline Prinsloo / GCIS / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES
Viongozi wa mataifa ya Afrika wakiwa katika mkutano mjini Addis AbabaPicha: picture-alliance/dpa

"Marais wote walioalikwa wamekubali ama kuhudhuria ama kutoa mamlaka ya kutia saini," taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Ijumaa ilisema. Umoja wa Mataifa unatarajiwa kumteua mjumbe maalum kuangalia utekelezwaji wa makubaliano hayo. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa hali ya kutokubaliana mwezi Januari ilitokana na wasi wasi juu ya utaratibu, lakini sio kutokana na muktadha wa makubaliano hayo.

Makubaliano hayaeleweki

Jason Stearns, mchambuzi binafsi ambaye hufuatilia masuala ya Kamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, mapema mwezi huu ameyaita makubaliano hayo kuwa ni "waraka usioeleweka kabisa, wenye kurasa mbili."

Makubaliano hayo, amesema, yanalenga katika vipengee vitatu: "kuzuwia mataifa ya eneo hilo kuingilia masuala ya ndani ya kila nchi, kuhimiza kufanyiwa mageuzi taasisi dhaifu nchini Congo na kuvutia hali bora zaidi kwa wafadhili na uhusishwaji.

Eneo la mashariki ya Kongo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini limeharibiwa na makubdi kadha yenye silaha katika muda wa miongo miwili iliyopita, huku makundi mapya ya waasi yakizuka kila mara, baadhi yao yakiungwa mkono kutoka katika nchi jirani.

M23 rebels withdraw from the Masisi and Sake areas in the eastern Congo town of Sake, some 27 kms west of Goma, Friday Nov. 30, 2012. Rebels in Congo believed to be backed by Rwanda postponed their departure Friday from the key eastern city of Goma by 48 hours for “logistical reasons,” defying for a second time an ultimatum set by neighboring African countries and backed by Western diplomats. The delay raises the possibility that the M23 rebels don’t intend to leave the city they seized last week, giving credence to a United Nations Group of Experts report which argues that neighboring Rwanda is using the rebels as a proxy to annex territory in mineral-rich eastern Congo.(Foto:Jerome Delay/AP/dapd).
Waasi wa kundi la M23 wakiondoka kutoka mji wa Goma mwaka janaPicha: AP

Ongezeko la hivi karibuni la machafuko lilitokea mwaka 2012 na kusababisha kuzuka kwa kundi la waasi la Machi 23, (M23) ambalo kwa muda lilikamata mji muhimu wa Goma Novemba mwaka jana. M23 liliundwa na wapiganaji wa zamani wa kundi la waasi wa kabila la Watutsi, ambao wanachama wake waliingizwa katika jeshi la kawaida la serikali ya Congo chini ya makubaliano ya amani ambapo masharti yake wanadai hayakutimizwa.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Iddi Ssessanga