1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ving'ora vya tahadhari vyalia kote Ukraine Ijumaa

Hawa Bihoga
3 Februari 2023

Ving'ora vya tahadhari vimelia kote nchini Ukraine leo Ijumaa, wakati Rais Volodymyr Zelenskiy akiwakaribisha viongozi wa Umoja wa Ulaya

https://p.dw.com/p/4N4mh
Von der Leyen mit EU-Kommission zu Gesprächen in Kiew
Picha: Uncredited/Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa/picture alliance

Hayo yamejiri wakati viongozi hao wakitarajiwa kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi, na matarajio ya Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo hakukuwa na ripoti za mara moja kuhusu mashambulizi mapya kufautia tahadhari hizo za mashambulizi ya angani.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya na Mwenyekiti wa viongozi 27 wa mataifa ya umoja huo, walikuwa mjini Kyiv kuonyesha uungaji mkono kwa Ukraine, wakati ambapo uvamizi wa Urusi ulioanza Februari 24, 2022 ukikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili.

Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya wameapa kuendelea kuiunga mkono Ukraine, huku rais Zelenskiy akitaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya Urusi, na kutaka kuanzishiwa mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Serikali ya Ujerumani pia imeidhinisha upelekaji wa vifaru chapa ya Leopard 1 na pia iko katika mazungumzo na Qatar, kununua vifaru tena 15 aina ya Gepard ilivyoiuzia Qatar, ili kuvituma nchini Ukraine.