VILNIUS:Marekani na Ufaransa zimetofautiana juu uwezekano wa jukumu la shirika la NATO katika eneo la mzozo la Dafur nchini Sudan.
22 Aprili 2005Tofauti hizo zimeibuka wakati wa mkutano wa mataifa wanachama wa shirika la NATO nchini Lithunia, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice alisema muungano huo unafaa kuwa tayari kutoa usaidizi katika eneo la Darfur iwapo utatakiwa kufanya hivyo. Lakini waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Michael Barnier alisisitiza kwamba NATO sio polisi wa ulimwengu.
Alitilia mkazo kwamba umoja wa Afrika uendelee kushikilia kuongoza juhudi za mpango wa amani katika eneo hilo.
Wakati huo huo NATO imetia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Russia. Shirika hilo pia limetoa vigezo vipya vya kuimarisha uhusiano wake na Ukraine. Marekani na Russia zilitofautina pia juu ya suala la Belarus baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice kuitaja Belarus kama nchi ya pekee ya Ulaya yenye uongozi wa kidikteta.