1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VILNIUS. Rice akutana na mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya shirika la NATO.

21 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKx

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amefanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa shirika la NATO mjini Vilnius, nchini Lithunia. Mkutano huo mkubwa wa kwanza kuwahi kufanyika katika taifa hilo la zamani la kisovieti, ulijadili mpango wa kuiruhusu Ukraine kujiunga na shirika la NATO.

Lakini maafisa wa NATO wamesema huenda wasiweke tarehe maalumu ya Ukraine kujiunga na shirika hilo kwa hofu ya kuikasirisha Russia. Hata hivyo Russia inashiriki katika mazungumzo hayo na serikali ya Moscow bado inaonekana kama mshiriki wa NATO.

Condoleezza Rice aliwasili Vilnius akitokea Russia ambako alikutana na rais Vladamir Putin na waziri wa mambo ya kigeni, Sergei Lavrov. Aliwaambaia waandishi habari mjini Moscow kwamba Marekani ina wasiwasi kuhusu demokrasia na haki za binadamu nchini Russia, na kumlaumu Putin kwa kulimbikiza madaraka katika ikulu ya Kremlin.