VILNIUS. Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO wakutana nchini Lithuan.
22 Aprili 2005Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa NATO wamekamilisha siku yao ya kwanza ya mkutano wa kihistoria unaoendelea kwa mara ya kwanza katika mji ambao hapo zamani ulikuwa chini ya utawala wa kisovieti mji wa Vilnius, nchini Lithuan.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ambae anahudhuria mkutano huo kama mgeni mualikwa ametia saini mkataba wa maelewano na katibu mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer.
Mkataba huo utarahisisha mpango wa kufikisha misaada kwa vikosi vya kulinda amani vya ISAF huko Afghanistan vinavyo ongozwa na umoja wa NATO.
Lakini Sergei Lavrov amekatalia mbali wito wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice wa kutaka mabadiliko ya uongozi huko Belarus kwa kusema kuwa serikali ya Moscow haitajihusisha kamwe na mabadiliko ya taifa lolote lile.