1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Villa akana madai ya unyanyasaji wa kingono

23 Julai 2020

Mchezaji wa kimataifa na mfungaji bora katika vilabu vya nchini Uhispania David Villa amekanusha madai ya udhalilishaji wa kingono wakati akiwa mchezaji wa klabu ya soka ya New York.

https://p.dw.com/p/3fpaE
FIFA Confederations Cup
Picha: picture-alliance/dpa/Photoshot

Madai hayo yalitolewa wiki iliyopita na msichana mmoja aliyesema alidhihakiwa kijinsia na Villa, wakati akiwa mafunzoni kwenye klabu hiyo ya New York City, wakati mwanasoka huyo alipokuwa akicheza na klabu hiyo kati ya mwaka 2015-18.

"Ninakanusha vikali madai hayo yanayotolewa dhidi yangu kupitia kwenye mtandao wa twitter" amesema Villa ambaye amestaafu soka katika taarifa yake iliyowasilishwa na wakala wake kwenye kituo cha utangazaji wa habari za michezo cha ESPN. Amesema "Madai hayo ni uongo mtupu na ninayakana".

Klabu hiyo ilitoa iltoa taarifa siku ya jana Jumatano kwamba ambayo ilisema kwamba inalichukulia suala hilo kwa "umakini mkubwa" na imeanzisha uchunguzi wake dhidi ya madai hayo. "Hatukubaliani na aina yoyote ya unyanyasaji katika idara yoyote ya klabu yetu", klabu hiyo imesema.

"Unyanyasaji ni tatizo kubwa kwa watu wengi," imesema taarifa ya Villa iliyotolewa na ESPN. Amesema, alisikia tu taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii, lakini hakupata simu kutoka kwa ESPN wala mhanga mwenyewe ama klabu ya New York City.

Msichana huyo amesema kwamba Villa alikuwa "akimgusa kila....siku" ambayo alifanya kazi klabuni hapo, na kuwasilisha malalamiko kwa wakuu wa klabu ambao hata hivyo hawakuchukua hatua zozote. Badala yake walidhani kwamba ulikuwa ni "mchezo tu wa kuigiza", alisema.

Mashirika: DPAE