1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vilabu vya Ligi ya Soka Ufaransa kugoma

25 Oktoba 2013

Vilabu vya kabumbu nchini Ufaransa vitafanya mgomo mwezi ujao wa Novemba kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kulalamikia mipango ya serikali kuwatoza kodi ya asilimia 75 wanaopata mapato makubwa

https://p.dw.com/p/1A6Jh
Wachezaji wa klabu ya Ufaransa Paris St. Germain wakishangilia na mashabiki wao baada ya mchuawano
Wachezaji wa klabu ya Ufaransa Paris St. Germain wakishangilia na mashabiki wao baada ya mchuawanoPicha: Reuters/Robert Pratta

Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972 unatarajiwa kuandaliwa katika wikendi ya mwisho ya Novemba baada ya vilabu vya nchini humo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo wenye utata wa Rais Msoshalisti wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza kiwango kikubwa cha kodi.

Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel amesema hakutakuwa na mechi mnamo tarehe 29 Novemba na Desemba 2. Chini ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi waoambao ni wachezaji ambacho kinazidi euro milioni moja.

Louvel anasema vilabu ambavyo vina wasiwasi kuwa uwezo wao wa kuwavutia wachezaji mahiri wanaopata mishahara minono kutoka ng'ambo kucheza nchini Ufaransa utakwama, vitafungua milango yao kwa mashabiki kufafanua kwa wafuasi wao ni kwanini wanahitaji kuchukua hatua hizo kali.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/reuters

Mhariri: Yusuf Saumu