1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vyarefushwa

21 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFc7

Brussels:

Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Umoja wa Ulaya wakikutana mjini Brussels, Ubelegiji leo wameafiki kurefusha vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe kwa mwaka mmoja zaidi. Mawaziri hao hata hivyo, watatathmini tena uamuzi wao, ambao umeingia mwaka wa nne sasa, baada ya uchaguzi mkuu utakaofanywa nchini humo mwezi ujao. Vikwazo vinahusu silaha, safari na kuzuia fedha za Watu wanaoshukiwa kuvunja haki za binaadamu nchini Zimbabwe. Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wamechukua uamuzi huo wakipinga utawala wa kimabavu unaoendeshwa na Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe.