1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya usalama Iraq wafanya mashambulizi

3 Januari 2014

Vikosi vya usalama nchini Iraq vimepigana na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la Al-Qaida walioivamia miji inayokaliwa na wasunni, pamoja na kuviteka vituo vya polisi katika mkoa wa al-anbar.

https://p.dw.com/p/1Akl2
Gari aina ya Pickup yaripuka katika eneo kuu la kibiashara.
Gari aina ya Pickup yaripuka katika eneo kuu la kibiashara.Picha: picture-alliance/AP Photo

Miji miwili iliyotekwa ni pamoja na Fallujah na Ramadi ambayo yote inakaliwa na wakaazi wengi wa madhehebu ya Sunni, ambayo imewahi kuwa ngome ya wanamgambo wa vikosi vya usalama kutoka Marekani.

Vikosi hivyo vya wanamgambo viliwavamia wapiganaji kwa maroketi ambayo yalitolewa na serikali ya Marekani kusaidia mapambano dhidi ya kikundi cha waasi wa Al-Qaeda cha Iraq, ambacho pia kinafanya mashambulizi katika mpaka wa Syria.

Tawi la wanamgambo wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda huko Iraq walionekana kutaka kulipiza kisasi kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa ngazi za juu wa madhehebu ya Sunni wikili iliyopita, kwa madai ya kufanya ugaidi.

Kukamatwa kwa kiongozi huyo, kuliamsha mapamabano mapya na hivyo kuendelezea mapigano yaliyodumu kwa mwaka mmoja sasa , tangu Marekani ilipoondoa majeshi yake kutoka Iraq.

Eneo la kibiashara laripuliwa

Vurugu hizo zilianza katika eneo la Anbar, wakati gari aina ya Pick up liliporipuka katika eneo kuu la kibiashara jana jioni katika mji wa Balad Ruz, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Baghdad, na kuharibu maduka kadhaa.

Miji ya Ramadi na Fallujah yenye wakaazi wengi wa madhehebu ya Sunni yavamiwa.
Miji ya Ramadi na Fallujah yenye wakaazi wengi wa madhehebu ya Sunni yavamiwa.Picha: Reuters

Katika mripuko huo, takribani watu 19 wameripotiwa kuawa na wengine 37 kujeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa maafisa usalama ambao hawakutaka kutaja majina yao, kwa madai kuwa hawakuruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine, vikosi vya serikali vimeshambulia katika mji wa Baghdad na kufanikiwa kuukoa mji mmoja, uliokuwa umetekwa na wapiganaji hao.

Katika makubaliano na wasunni, Waziri Mkuu Nuri al-Maliki anayeongoza kambi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ameviondoa vikosi vya wanamgambo kutoka katika eneo la Anbar na kuwaachia askari wa kawaida kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Washia wanadai kutengwa

Kambi ya madhehebu ya Shia imekua ikipamabana na serikali tangu kuanza kwake mwaka mmoja uliopita kutokana na kile wanachokiona kwamba wanatengwa kwa tofauti ya kimadhehebu.

Watu elfu nane nchini Iraq wameripotiwa kuuawa mwaka huu.
Watu elfu nane nchini Iraq wameripotiwa kuuawa mwaka huu.Picha: Reuters

Lakini mara tu baada ya kuondoka katika mji huo, wanamgambo hao wamehamishia mashambulizi yao katika mji hiyo miwili ya Ramadi na Fallujah, na miji mingine miwili ya karibu.

Idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni wamekuwa wakilalamika kwamba Washia wanatawala kimabavu tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Saddam Hussein mwaka 2003. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu elfu nane wameuwawa mwaka huu pekee kutokana na machafuko nchini Iraq.

Mwandishi: Flora Nzema/APE

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman