Vikosi vya Umoja wa Afrika kubakia Somalia
22 Februari 2008Matangazo
NEW YORK:
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeidhinisha azimio kuruhusu kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika kuendelea kubakia nchini Somalia kwa miezi sita mingine.Muda huo unatoa nafasi kwa Umoja wa Mataifa kuzingatia mpango wa kupeleka vikosi vyake vya amani katika nchi hiyo.
Azimio hilo linazihimiza nchi za Kiafrika kusaidia kifedha na kutoa misaada mingine kwa kikosi hicho kidogo cha Umoja wa Afrika kinacholinda amani nchini Somalia tangu mwezi Machi mwaka 2007.Somalia,kila siku inashuhudia mapambano kati ya wanamgambo wa Kiislamu,wababe wa vita na vikosi vya Somalia vinavyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia.