1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya NATO kwa Mashariki ya kati ndio mada kuu

Ramadhan Ali25 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CHVR

Tukianza na BERLINER ZEITUNG linahisi kuwa kutumika kwa vikosi vya NATO nchini Lebanon kuhifadhi amani kumehitaji kuregeza kamba mno kwa wafuasi wake wakubwa:Marekani na Israel.

Berliner zeitung laandika:

“vikosi vya shirika la ulinzi la NATO vitaweza tu kufanikiwa kwa muda mrefu kutuliza hali ya mambo ikiwa tu serikali ya Israel mjini Jeruselem itakuwa tayari kuwaridhia madai yao majirani zake na wapalestina.Kufikia shabaha hiyo,haitawezekana bila shinikizo kutoka Marekani.Kwahivyo, kuleta utulivu kijeshi kusini mwa Lebanon lazima kuaandamane na juhudi kubwa za kuleta ufumbuzi wa amani katika Mashariki ya kati kutoka kwa Marekani.Ni kwa jicho hilo tu,kutuma majeshi huko ya NATO kutakua na maana-“laandika gazeti.

Gazeti linalochapishwa mjini Munich ABENDZEITUNG-lasema Israel sasa imetambua hali hasa ilivyo:

“Kwa kuzinduka serikali ya Israel imechangia mno kubadilika kwa sura ya mambo:kwani hadi sasa kidole kikinyoshewa wapalestina tu kuwa ndio wakorofi waliotaka kutapakaza mgogoro huu duniani.Waisraeli wakitaka tuz silaha za Marekani na halafu waachiwe wafanye watakavyo.Hii haiwezekani tena.”

Likiendelea laandika,

“Licha ya wasi wasi wote uliopo waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Bw. Jung haoni taabu yoyote vikosi vya NATO kupelekwa nchini Lebanon.Licha ya historia ya siku za nyuma ya wajerumani na wayahudi,fikra ya kutumwa vikosi hivyo isitupiliwe mbali ikiwa tu itachangia kuhifadhi amani.”-ni maoni ya ABENDZEITUNG kutzoka Munich.

Likiendelea na mada hii ya kushirikishwa kwa wanajeshi wa Ujerumani kuhifadhi amani katika mashariki ya kati,gazeti la OFFENBURGER BLATT laandika:

“Kushiriki kwa vikosi vya Ujeruimani kuhifadhi amani mashariki ya kati ni lazima kwa sababu historia ya Ujerumani ya MANAZI inaonesha yapaswa kuwapo mpaka wa kuvumiliana.Kwani, anaekiuka haki za binadamu na kuzikanyaga na yule anaetaka kulihilikisha taifa jengine, huyo yuko nje ya mipaka ya jamii iliostaarabika….Mikasa kama hii imeonekana Bosnia,Kosovo,Afghanistan,K ongo na kwahivyo pia hata Lebanon.Kwani, vitimbi tangu vya waisraeli hata vya wa-hizbollah vimevuka mpaka wa kiwango cha kuvumiliwa.”

Likituhetimishia mada hii, gazeti la TAGESPOST kutoka Würzburg linaonya:

“Pengine vikosi vya ulinzi vya Umoja wa Ulaya vitawekwa kuzitenganisha pande mbili zinazopigana huko Mashariki ya kati.Mashariki ya kati lakini, sio Kongo.Kwani, kutuma vikosi huko si kazi ya muda mfupi.

Na kwahivyo, si sawa kutuma huko vikosi vya UU.Wanajeshi pekee hawawezi kufumbua kitandawili hiki. Umoja wa Ulaya kwahivyo, unapaswa kushughulikia ufumbuzi wa kisiasa wa mzozo huu.Haufanyi hivyo,wanajeshi wake watajikuta wanapambana na changamoto nyengine kabisa-Syria na Iran.”