1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Israel vyamuua kamanda wa Hamas mjini Jenin

30 Agosti 2024

Vikosi vya Israel vimemuua kamanda wa Hamas katika mji wa Jenin ambao ni kitovu cha mapigano hivi sasa, wakati jeshi hilo likiendeleza operesheni yake kwenye eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4k7K2
Gaza | Nuseirat
Mushi unafuka hewani baada ya shambulio la Israel katika eneo la kambi ya wakimbizi wa Palestina Nuseirat.Picha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Jeshi limesema kikosi cha Polisi wa Mipakani kilimuua kamanda huyo Wassem Hazem, anayedaiwa kuwa mkuu wa Hamas huko Jenin na anayehusishwa na mashambulizi katika eneo la Palestina.

IDF aidha limesema wapiganaji wengine wawili wa Hamas waliojaribu kukimbia pia waliuliwa na droni na kuongeza kuwa silaha, vilipuzi na kiasi kikubwa cha fedha vilikutwa kwenye gari lao.

Soma pia:Israel yathibitisha kumuua kamanda wa Fatah

Hamas imethibitisha vifo vya watu hao watatu na kusema walikuwa na wanamgambo wa tawi lake la kijeshi la Al-Qassam.