1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ethiopia vyachukua udhibiti wa mji wa Lalibela

20 Desemba 2021

Shirika la habari la serikali nchini Ethiopia limeripoti kuwa Jeshi la nchi hiyo limechukua tena udhibiti wa mji wa Lalibela, maarufu kwa makanisa yaliyochongwa kwa mawe.

https://p.dw.com/p/44YdM
Äthiopien | Norden | Rebellen Tigray
Picha: S.Getu/DW

Shirika hilo la habari limeonyesha picha za naibu waziri mkuu akitembelea eneo hilo.

Hata hivyo, haijafahamika ni lini vikosi vya serikali vilichukua udhibiti wa mji huo, ulio na umuhimu mkubwa kwa Wakristo wa kiorthodox.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa Tigray waliuteka mji huo mnamo mwezi Agosti lakini vikosi vya serikali vilikabiliana na waasi hao mwanzoni mwa mwezi Disemba na kulazimisha waasi hao kuondoka.

Mzozo wa mwaka mmoja kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya serikali umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha maelfu ya wengine wakikabiliwa na baa la njaa.