Vikosi vya Australia kuondoshwa Irak hatua kwa hatua
30 Novemba 2007Matangazo
Australia inatazamia kuwarejesha nyumbani kama wanajeshi 550 kutoka Irak ifikapo katikati ya mwaka 2008.Hivi sasa Australia ina wanajeshi 1,500 nchini Irak,kama sehemu ya vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na Marekani.
Waziri Mkuu mteule Kevin Rudd wakati wa kampeni ya uchaguzi,aliahidi kuwarejesha nyumbani wanajeshi hao hatua kwa hatua.